Vigezo na Masharti


SEHEMU YA I 

UTANGULIZI

 

LENGO:

Hati hii inakusudiwa kutowa ufafanuzi wa vigezo na masharti kwa watumiaji wa huduma za EzyPesa. 

 

ENEO:

Hati hii itasaidia kuhakikisha kwamba fedha za watumiaji wa huduma na mawakala zinalindwa na vilevile kampuni ya Zantel inapata kinga kwa hatua inazochukua kulinda maslahi yake. 

 

UFAFANUZI:

“Wateja” maana yake ni mtu yeyote anaeingia katika mkataba wa kupata huduma za mawasiliano kutoka Zantel.

“Wakala” maana yake ni wakala aliyesajiliwa kutoa huduma.

“Wafanya Biashara” ni watowa huduma waliounganishwa na mfumo wa EzyPesa kama njia ya ukusanyaji wa malipo ya stakabadhi ya huduma. 

“Simu ya Mkononi” maana yake ni pamoja na kifaa au mchanganyiko wa vifaa vinavyomuwezesha mtumiaji kupata huduma ya mawasiliano ya simu kupitia mtandao wa Zantel.

“SIM Card” maana yake ni kadi inayomilikiwa na Zantel anayopewa mteja kwa mawasiliano.

“Huduma” maana yake ni huduma ya Ezypesa au huduma nyengine yoyote ya mawasiliano inayotolewa na Zantel.

“Viwango vya bei” maana yake ni ada, tozo au viwango vya gharama ambavyo huweza kubadilika mara kwa mara. 

“KYC” ni ufupisho wa maneno ambayo yanakusudiwa kuwa na maana ya “kumjua mteja wako” katika utaratibu mzima wa kibiashara na uhakiki wa wateja kwa ajili ya kuthibitisha uhalali wa wateja.

“Pasiwadi au Nywila” maana yake ni neno au mchanganyiko wa herufi na namba zenye kutambulisha uhalali wa mteja ili kuweza  kuingia katika mtandao au kompyuta ambayo inawekwa kuwa ni siri kwa watu wasiohusika. 

 “Utakasaji wa fedha haramu” maana yake ni utaratibu wa kugeuza(kuhalalisha) mali au pesa ziliyopatikana kinyume na sheria 

“Mapambano ya Utakasaji wa Pesa (AML)” maana yake ni sheria, kanuni, sera, taratibu na udhibiti ambao umewekwa kwa madhumuni ya kuzuia wahalifu kutumia mfumo wa pesa kuficha uharamu wa pesa zao.

“Mapambano ya  Uchangiaji pesa Maharamia” maana yake ni sheria, kanuni, sera, taratibu na udhibiti ambao umewekwa kwa makusudi ya kuzuia kuwawezesha kifedha magaidi

AINA ZA WADAU:

  • Wateja 
  • Mawakala Wakubwa
  • Mawakala
  • Wafanya Biashara

 

 

SEHEMU YA II 

WAJIBU WA MTEJA

 

1.1 Mteja anatakiwa awe na SIM iliyo halali na iliyosajiliwa ipasavyo iliyotolewa kwa mujibu wa kanuni za kumjua mteja pamoja na sheria na kanuni nyengine kuhusiana na usajili wa simu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanania  kama zitakavyorekebishwa mara kwa mara.

1.2 Kutoa taarifa kwa Zantel haraka iwezekanavyo panapotokea wizi au upotevu wa SIM card.

1.3 Kutoa taarifa kwa haraka Zantel pale panapokuwa na wasiwasi au tuhuma za vitendo vya utakasaji wa fedha haramu.

1.4 Haraka kuiarifu Zantel baada ya kugundua wizi, ulaghai, upotevu, matumizi yasiyoruhusiwa au tukio jengine lolote haramu kuhusu akaunti/masuala ya EzyPesa. 

1.5 Kuwa makini kwa usalama na usiri wa pasiwadi.

1.6 Pasiwadi (Nyila) ni siri yako usimpe/kumuonyesha mtu yeyote 

 

 

SEHEMU YA III 

WAJIBU WA ZANTEL

 

2.1 Zantel kwa haraka itaifunga SIM Card iliyopotea, iliyoibiwa au iliyoharibika ili kuzuia mawasiliano mara tu baada kupokea taarifa kutoka kwa mteja. 

2.2 Bila ya taarifa au kuridhia kwa mteja, Zantel kwa haraka itaifunga akaunti yoyote ya Ezypesa pale mteja/mtumiaji atakapoingiza pasiwadi au taarifa nyengine zisizo sahihi kwa zaidi ya mara tatu wakati akitumia huduma ya EzyPesa.

2.3 Akaunti yoyote ya EzyPesa iliyofungwa inaweza kufunguliwa baada ya masaa 48.

2.4 Zantel haitokuwa dhamana wa hasara yoyote itakayopatikana kutokana na kushirikiana kusiko halali katika matumizi ya pasiwadi.

2.5 Zantel inawajibika kufikisha  taarifa kuhususiana na miamala  yenye  mashaka ya  utakasishaji wa fedha haramu katika mamlaka husika.  

 

Angalia Kama Unapata Huduma

Tafuta duka la Zantel