Uwajibikaji wa Kijamii


Hapa Zantel uwajbikaji wetu wa kijamii ni jinsi ni biashara inavyofanyika kwa kuhusisha shughuli zinazoendelea kwa maadili na kwa haki na inis inavyoathiri jamii inayotuzunguka. 

Dira yetu ya uwajibikaji ni kutengeneza mazingira endelevu ya kiuchumi na ya kijamii yenye upatikanaji bila kikomo.

Dhamira yetu ya uwajibikaji ni kupanua upatikanaji kwa watanzania kwa kuwapa bidhaa na huduma zenye manufaa katika jamii; kuwezesha ukuaji endelevu kupitia miradi mbali mbali, kukuza vipaji, kusaidia jamii, elimu, afya na kujenga uhusiano wa maana na wadau kupitia ushirka - dalili ya kua matumaini na mtazamo wa kujali huvunja mipaka yote.

Programu za Kusaidia Jamii

Zantel inaendelea kusaidia jamii kupitia programu hii

  • Zantel ilichangia vitabu vyenye thamani ya milioni TZS 10 katika maktaba ya Zanzibar (ZLS) na kukuza usomaji na upatikanaji kwa wanaotumia maktaba katika visiwa hivyo.
  • Zantel ilichukua darasa la walemavu wa kuona na kuchangia vifaa vyenye thamani ya milioni TZS 20 kwa shule ya msingi ya Kisiwandui iliopo Ugunja.

 

Angalia Kama Unapata Huduma

Tafuta duka la Zantel