Kuhusu Zantel


Zantel inatoa huduma za mawasiliano zenye ubora wa hali ya juu nchini Tanzania kwa thamani ya fedha ya watumiaji, wafanyabiashara na watoa hudumaza mawasialiano wengine.

Zantel inajivunia katika mfumo thabiti wa huduma zake kupitia huduma za simu ikiwemo maongezi na huduma za  mtandao mkubwa wa 4G nchini Tanzania, pamoja na huduma zake za kifedha za simu maarufu kama “Ezypesa”, Zantel pia inaongoza katika utoaji wa huduma bora ya intaneti kwa wafanyabiashara nchini Tanzania pamoja na kutoa huduma za simu za kimataifa na intaneti kwa watoa huduma wengine wakubwa wa mawasiliano nchini Tanzania.

Zantel ni moja kati ya makampuni yanayomilikiwa na Millicom. Milicom ni kampuni ya mawasiliano ya simu na utoaji taarifa inayoongoza ambayo imejikita katika masoko yanayo chipukia Amerika Kusini na Afrika. Millicom hujipanga na kasi ya ubunifu wa utoaji wa huduma za kidigitali zinazoendana na maisha ya wateja wake katika masoko chipukizi.

Millicom Group imeanzishwa mwaka 1990, imeajiri zaidi ya wafanyakazi 16,000 na inahudumia zaidi ya wateja Milioni 62. Millicom International Cellular ina makao yake makuu Luxemborg nchini Afrika kusini na imeorodheshwa kwenye NASDAQ OMX Stockholm chini ya jina la MIC.

 

Kuhusu Zantel

Angalia Kama Unapata Huduma

Tafuta duka la Zantel