ZANTEL YAZINDUA VIFURUSHI VYA BURE KWA MITANDAO YOTE YA KIJAMII ILI KUWANUFAISHA VIJANA


 Kampuni ya simu inayoongoza kwa huduma za vifurushi vya intaneti, Zantel imeanzisha huduma mpya ya vifurushi vya bure kwa wateja wake ikiwalenga zaidi vijana, ambapo tafiti zinaonyesha ndio watumiaji wakubwa wa mitandao ya kijamii.

Akizindua rasmi huduma hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Bw. Benoit Janin amesema wateja wa Zantel wanaojiunga na vifurushi vyetu vya kila siku, wiki na mwezi watapata nafasi ya kutumia mitandao ya Facebook, Twitter pamoja na huduma ya kusikiliza muziki bure kwenye application ya ‘Mdundo.com’.

Aliongeza kwa kusema “Tunajisikia fahari kubwa sana kuweza kuzindua huduma hii mpya ikiwa ni mwendelezo wa jitihada zetu za kupanua na kutoa huduma za kibunifu na kuhakikisha wateja wetu wanaendelea kufurahia mtandao wetu wa Zantel wenye huduma ya intaneti ya kasi zaidi ya 4G Tanzania nzima.

Akifafanua zaidi kuhusu huduma hiyo, Mkuu wa kitengo cha huduma ya Vifaa na intaneti Zantel, Hamza Zuberi alisema, “Kwa wateja wa Zantel watakaonunua vifurushi vya siku, wiki na mwezi ambavyo ni ;-Sh.500/= kwa 500MB, Sh.1000/= kwa 1.2GB, na Tsh.1500/= kwa 2.5G watapata nafasi ya kufurahia huduma hizo za bure. Huduma hizi ni kwa wateja wenye simu au vifaa vyenye uwezo wa kupokea huduma ya intaneti. Kwa wateja wetu wanaotumia simu au vifaa visivyo na uwezo huo wanaweza kujipatia simu au vifaa hivyo kwa gharama nafuu kabisa katika maduka ya Zantel jijini Dar es Salaam na visiwani Zanzibar ili na wao waweze kufurahia ofa hii”.

Aliongeza kuwa baada ya kufanya utafiti wa kina kwenye soko la mitandao ya simu waligundua kuwa vijana wengi wanapenda muziki ambapo mpaka sasa hakuna kampuni yoyote ya simu inayotoa huduma hiyo bure, na hivyo kuwafanya Zantel kuileta huduma hiyo sokoni kwa kupitia ‘Mdundo Music Application.’

‘Mdundo Music Application’ ni moja ya programu kubwa kabisa za muziki barani Afrika inayowawezesha watu kuweza kusikiliza aina zote za muziki kwa kutumia intaneti. Programu hiyo ina zaidi ya nyimbo 200,000 kutoka kwa wanamuziki zaidi ya 40,000. Zantel inaamini ofa hii itawafaa zaidi vijana kwakuwa wengi wao wamekuwa kwenye utamaduni wa kisasa unaopenda zaidi muziki na hivyo huduma hii ya bure itawavutia zaidi.

Aliongeza kuwa huduma hiyo mpya inapatikana karibu kwenye mifumo yote ya simu za mkononi kama vile Android, iOS kwa ajili ya iPhone, Blackberry na Nokia Symbian.

Prisna Nicholaus , Meneja wa muziki na uendeshaji wa Mdundo.com alisema, "Wateja wa Zantel wanaweza kupata orodha yote ya nyimbo kupitia Mdundo ikiwa ni pamoja na nyimbo mchanganyiko zilizoandaliwa na Ma DJ maarufu, muziki wa Afrika Magharibi na pia Mashariki. Tanzania ni soko letu ambalo linakuwa kwa kasi sana na tunatarajia kuwa mpango huu utasaidia kupunguza kiwango kikubwa cha uharamia kwenye soko la muziki nchini na kuwapa wateja sababu ya kufurahia muziki zaidi ya hapo awali”.

Huduma hii mpya kutoka Zantel imekuwa miongoni mwa huduma nyingine za kibunifu na kidijitali ambazo zimeanzishwa na Kampuni hiyo hivi karibuni. Huduma hizo ni pamoja na uzinduzi wa mtandao wenye kasi wa 4G LTE upande wa Bara na Visiwani, 'Zantel Madrasa' huduma inayowawezesha waumini wa dini ya Kiislamu kupata mafundisho, Quran, Habari za BAKWATA na mawaidha mbalimbali ya kiislamu kwa njia ya simu, ikiwemo pia kwa njia ya SMS na ‘ Zantel Madrasa App’.

Akizungumzia uwekezaji wa Zantel, Janin alisema wamewekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 10 katika uboreshaji wa mtandao ambapo mpaka sasa zoezi la maboresho hayo katia maeneo ya Stone Town Zanzibar na Mkoa wa Mjini Magharibi yameshakamilika. Zoezi hilo linaloendelea hivi sasa katika visiwa vya Unguja na Pemba linaarajiwa kufikia kikomo mwisho wa mwezi huu.

Kwa maelezo zaidi, tutumie ujumbe

Angalia Kama Unapata Huduma

Tafuta duka la Zantel