Zantel yazindua promosheni ya watumiaji wa huduma ya EzyPesa


Dar es Salaam, Februari 6,2019 : Kampuni ya mawasliano Zantel, leo imezindua promosheni kwa watumiaji wa huduma yake ya kifedha ijulikanayo kama EzyPesa ili kuwezesha wateja wake kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu.

Promosheni hii itakayodumu kwa kipindi cha miezi mitatu, ni rasmi kwa ajili ya wateja wote wanaotumia Ezypesa pamoja na wateja wapya wanaoendelea kujiunga na huduma hio. Kila mara mteja atakapo tuma ama kupokea fedha kupitia EzyPesa, atajiweka kwenye nafasi ya kujishindia zawadi nono kama simu za mkononi zinazotumia interneti (Smartphones) na fedha taslimu kuanzia shilingi 200,000/- hadi shilingi 1,000,000/-

Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bidhaa na Huduma wa Zantel, Aneth muga,, alisema promosheni hii itawezesha watumiaji wa huduma ya EzyPesa kujipatia motisha kama vile kurudishiwa fedha kwenye akaunti zao na kujishindia zawadi mbalimbali.

Watumiaji wa huduma ya EzyPesa watakaongeza salio la muda wa maongezi kuanzia shilingi 500/- watarudishiwa fedha zao. Wateja watakaotuma au kupokea kiasi cha shilingi 10,000/-wataingia kwenye droo ya wiki inayowezesha kujishindia simu ya kisasa (Smartphone). Kila wiki droo itakuwa na washindi 10 wa fedha taslimu na washindi 15 wa simu. Droo ya mwezi italenga kuwapata wateja 10 waliotuma na 10 waliopokea fedha kwa wingi.

EzyPesa ndio huduma pekee ya mtandao hapa Tanzania inayowezesha wateja wake kufanya miamala ya malipo ya kodi kwa ZBR na kununua umeme wa LUKU na TUKUZA. Huduma ya EzyPesa inaondoa adha ya wateja kupoteza muda mwingi wakipanga foleni ili kupata huduma za kibenki na kulipa ankra zao mbalimbali. Vile vile, EzyPesa sasa inapatikana katika program mpya ya simu za mkononi (Mobile Application) inayowezesha wateja kufanya malipo mbalimbali kwa njia rahisi zaidi.

Kwa sasa wastani wa miamala inayofanyika kwa mwezi kupitia huduma hii inafika million 5.6 na Zantel ina malengo ya kufikisha huduma hio kwa wateja 100,000 wapya kila mwezi. Zantel pia inaendelea kufanya majadiliano na taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo benki za CRDB na NBC kuhusu ushirikiano katika kutoa huduma za kifedha kupitia mtandao wake.

 

Angalia Kama Unapata Huduma

Tafuta duka la Zantel