Zantel yazindua kampeni ya ‘jero yako tu' kuwazawadia wateja wake


Januari 15, 2018. Zanzibar. Kampuni ya Mawasiliano ya ZANTEL, leo imezindua kampeni yake kabambe inayoitwa 'JERO YAKO TU', promosheni ambayo imelenga kuwashukuru wateja kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu.

Kampeni hiyo ambayo imeanza rasmi siku ya leo, itadumu kwa muda wa miezi mitatu huku takribani washindi 235 wakitarajiwa kuibuka na zawadi kabambe kutoka Zantel.

Zawadi kubwa katika promosheni hii itakuwa ni pamoja na magari matatu aina ya Suzuki Carry kwa washindi watatu, ambazo zitakabidhiwa mwishoni mwa kampeni hii mwezi Machi.

Zawadi za kila wiki ni pamoja na pikipiki 1, na baiskeli 4 huku zawadi za kila siku zikiwa ni simu aina ya smartphone 4G pamoja na fedha taslimu kiasi cha Sh. 50,000/= kila siku.

Kwa mujibu wa Zantel, Promosheni ya ‘JERO YAKO TU' ni mahususi kwa ajili ya kuwazawadia wateja na kuthamini uvumilivu wao wakati ambapo mtandao huo ulikuwa kwenye hatua za maboresho na hatimaye kuzindua mfumo wa 4G katika mikoa 22 nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mjini Zanzibar, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Sherrif El- Barbary  alisema, "Sisi Zantel tunathamini mchango wa wateja wetu ambao wametuonyesha kwa miaka mingi, na wanastahili kupongezwa kwa kuendelea kuwa nasi hususani kutufanya kuendeliea kuwa mtandao wa simu unaoongoza Zanzibar pamoja na kuongoza kwenye utoaji wa huduma ya data nchini Tanzania.

El Barbary Alisema, Ili kushiriki kwenye droo hiyo, cha kwanza anayeshiriki atapaswa kuwa na laini ya Zantel na kuweka salio la kuanzia shillingi 500 na moja kwa moja atakuwa ameingia kwenye droo. Aliongeza kuwa ili kujiwekea nafasi ya kushinda zawadi nono, mtumiaji atapaswa kuweka vocha mara nyingi kadri anavyoweza.

Aliongeza kuwa, "Ushindani kwenye soko umekuwa mkubwa na Zantel haina mpango wa kupunguza kasi na tunavyozungumza hivi sasa, tumeshamaliza zoezi la kuboresha vituo vyetu kwenda mfumo wa 3G na 4G kitu kinachoifanya Zantel kuwa kampuni ya mawasiliano iliyoonea nchi nzima.

Zantel imedhamiria kuwaweka mbele wateja wake kwa kuwaletea teknolojia mpya na ya kisasa pamoja na kuwa mtandao bora zaidi unaotoa suluhisho la huduma bora za data nchini Tanzania.

Kwa maelezo zaidi, tutumie ujumbe

 

Angalia Kama Unapata Huduma

Tafuta duka la Zantel