Zantel yazindua duka jipya eneo la Kariakoo-Jengo la China Plaza


Zantel yazindua duka jipya eneo la Kariakoo-Jengo la China Plaza, Hili likiwa ni duka la pili jijini Dar es Salaam na pia kuna vibanda vya huduma kwa wateja nchini kote na Jijini Dar es Salaam, Uzinduzi wa duka hili ni moja kati ya mipango ya kufungua maduka zaidi kwa wateja ili kupata urahisi kwa wateja kupata bidhaa za Zantel na huduma zake.

Wateja watapata uwezo wa kupata huduma mbalimbali ya vifaa ambayo vina teknolojia ya kisasa ya 4G, simu za kisasa na vifaa vingine kwa punguzo la bei hasa katika msimu huu wa sikukuu, pamoja na kujipatia mahitaji na huduma bora ya wateja.

Wateja wa Zantel pia kufurahia modem zenye vifurushi na huduma za wanafunzi na wafanyabiashara kwa bei nafuu zaidi, ili kuwasaidia kuungana na dunia popote pale walipo. 

Akizungumza katika uzinduzi wa duka hilo, Afisa Mkuu wa Zantel Benoit Janin alisema '' Ni furaha yangu kwa kuwakaribisha katika duka letu jipya hapa China Plaza- Kariakoo. Asante kwa wateja wetu kwa kutenga muda na kujiunga nasi katika uzinduzi wa duka letu jipya  na kituo cha huduma katikati ya mji ili kuwezesha kutumikia mamilioni ya watu ambao wana shughuli hapa Kariakoo. Tunaona fahari sana sisi kama Zantel kuleta bidhaa zetu nafuu na huduma bora Zaidi karibu na wateja wetu.

Kwa maelezo zaidi, tutumie ujumbe

 

Angalia Kama Unapata Huduma

Tafuta duka la Zantel