ZANTEL YATOA MSAADA WA SARUJI NA MABATI KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO WA MKOA WA KUSINI PEMBA


 

Pemba. Kampuni ya mawasiliano ya Zantel imetoa msaada wa mifuko ya Saruji na mabati kwa ajili ya waathirika wa Mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika Mkoa wa Kusini Pemba-Zanzibar.

Msaada huo ni pamoja na mifuko ya mia tatu hamsini (350) ya Saruji na mabati (350) ambao utasaidia kujenga baadhi ya nyumba zilizoathiriwa na mafuriko hayo.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Khamis Mussa (Baucha) alisema kampuni ya Zantel imeguswa sana na janga liliowakumba wananchi wa Pemba ambao wengi ni wateja wake na hivyo kuamua kuungana na Serikali katika kuwapa faraja wahanga.

Alisema katika kuhakikisha wananchi wanarudi katika makazi yao ya kawaida, Zantel itajitahidi kuhakikisha inakua pamoja na wananchi walioathirika ili waweze kurejesha makazi na hali yao ya kawaida.

“Tatizo la maafa ni la Watanzania wote sio Serikali peke yake hivyo na mimi naomba nitoe rai kwa wahisani na makampuni ambayo yameguswa na tatizo hili kujitokeza kwa wingi ili kukabidhi misaada yao”. Alisema.

Akipokea msaada huo, Mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdallah aliipongeza Zantel kwa kuwa kampuni ya kwanza kutoa msaada kwa wanananchi wake na kuziomba taasisi nyingine kujitokeza na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kurudisha furaha za wananchi wa Pemba.

“Ninawashukuru sana Zantel, siku zote mmekuwa mstari wa mbele katika kutupa msaada pale tunapokuwa tuna uhitaji. Mahitaji ya wananchi walioathiriwa na mafuriko bado ni mengi sana hivyo na mimi nitoe rai kwa wadau wengine kuja kutuungana mkono katika janga hili”. Alimalizia.

Kwa maelezo zaidi, tutumie ujumbe

Angalia Kama Unapata Huduma

Tafuta duka la Zantel