Zantel yatangaza muunganiko wao na Tigo


Dar es Salaam. November 1st, 2019. Kampuni ya simu za mkononi Zanzibar Telecom Public Limited Company (Zantel), leo, imetangaza kukamilika kwa mchakato wa kuungana na kampuni ya MIC Tanzania Public Limited Company (Tigo). Hii ni baada ya kupokea idhini kutoka mamlaka husika na sasa kampuni hizi mbili zinaungana na kuwa kampuni moja Tanzania Bara na Visiwani.

Akizungumzia juu ya suala hilo, Brian Karokola, Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Zantel, alisisitiza kwamba kampuni zote mbili zinakuja pamoja kwa lengo la kushirkiana na serikali kusogeza mbele maendeleo ya Tanzania: "Kupitia utoaji wa huduma bora kwa wateja, intaneti yenye kasi kubwa, mchanganyiko wa bidhaa zenye ubunifu wa hali ya juu na kuenea kwa huduma katika sehemu kubwa ya nchi, muunganiko wa kampuni hizi utaimarisha ushindani katika sekta ya mawasiliano ya simu kwa faida ya nchi kwa ujumla. Hakika hii ni habari njema kwa wateja wa Zantel ambao wataweza kupata huduma za hali ya juu za Tigo na kufaidika na bidhaa na huduma za kisasa na za hali ya juu."

Kuunganishwa kwa biashara hizi, kutaongeza nguvu kwenye makampuni haya mawili ya Zantel na Tigo katika kuhudumia vyema na kwa ubora zaidi wateja wetu walioko Zanzibar na Bara. Vilevile wateja watapata mawasiliano mazuri zaidi maeneo yote ya mijini na vijijini na kuwezesha pia upatikanaji wa suluhisho la mawasiliano kwa biashara mbalimbali pamoja na huduma za kifedha kupitia simu za mkononi kwa wateja wa Zantel na Tigo.

Uongozi wa Zantel na Tigo utahakikisha kuwa mchakato wa kuunganisha uendeshaji wa kampuni hizo mbili utawezesha wateja kuendelea kufurahia huduma zote za mitandao yao husika yani Zantel na Tigo bila matatizo yoyote. Namba na taarifa za wateja hazitabadilika na hakutakuwa na usumbufu katika upatiknaji wa mawasiliano, huduma na bidhaa wakati wote wa zoezi la kuunganishwa kwa kampuni hizi mbili.

Fact Sheet

Zantel na Tigo

Jumla ya Wateja: *12,883,000

Jumla ya Wateja wa Huduma za kifedha: *7,350,000

Kwanini kampuni za Zantel na Tigo zinaungana?

Kwa sasa soko la mawasiliano Tanzania limegawanyika sana hivyo kulikuwa na uhitaji wa kuunganisha makampuni haya. Kuunganishwa kwa shughuli za kiutendaji baina ya Zantel na Tigo kutaweka mazingira shindani na yenye tija kwa taifa, kutachochea maendeleo na ubunifu katika sekta ya mawasiliano na zaidi kuimarisha uwezo wa makampuni haya ili kuyawezesha kutoa huduma zenye ubora wa kimataifa kwa wateja wao waliopo Tanzania Bara na Visiwani.

Nini manufaa ya muunganiko huu kwa wateja, sekta ya mawasiliano na Taifa kwa ujumla.

  • Sekta ya mawasiliano: Kukuza na kuimarisha sekta, kuongeza uwekezaji na kuboresha huduma pamoja na kuchochea ubunifu
  • Kwa Taifa: kuchangia katika maendeleo ya Taifa kwa ujumla na katika sekta ya mawasiliano ya simu.
  • Kwa Wateja: Utaleta manufaa makubwa zaidi kwa wateja na biashara kwa ujumla kwa kuyafanya makampuni haya kupanua wigo wa uwekezaji na kuwapa wateja huduma bora zaidi, kuboresha upatikanaji wa mtandao na kukuza ubunifu na teknolojia.

Kutopatikana kwa huduma za mawasiliano wakati wa zoezi la kuunganisha shughuli za kiutendaji

Wateja wataendelea kufurahia huduma zote bila matatizo kutoka mtandao husika yaani Zantel au Tigo. Laini za simu na taarifa za wateja hazitabadilika na hakutakuwa na usumbufu katika upatikanaji wa mawasiliano na huduma nyingine.

Athari kwa Wafanyakazi

Kwa sasa, Zantel na Tigo zitaendelea kujiendesha kama kampuni tofauti na biashara zitaendelea kama kawaida. Wakati zoezi la kuunganisha makampuni haya mawili likiendelea, kutakuwa na uhamishaji wa rasilimali ndani ya Tigo na Zantel ambao hautaathiri shughuli za kiutendaji na tunategemea kutakuwa na athari ndogo tu kwa rasilimali watu (wafanyakazi) wa makampuni haya mawili.

Nini kitafuata?

Tunaendelea kuendesha biashara kama ilivyo ada na kwa sasa kila kampuni itafanya kazi zake kama taasisi inayojitegemea. Hata hivyo katika wiki zijazo zoezi la uunganishwaji wa shughuli za kiutendaji za makampuni haya utaanza na tutaendelea kutoa taarifa kwa wanahabari kuhusu hatua muhimu zitakazofikiwa wakati wa zoezi hili.

Angalia Kama Unapata Huduma

Tafuta duka la Zantel