Zantel Yakabidhi Msaada Wa Majenereta Kwa Taasisi Ya Karume Ya Sayansi Na Teknolojia, Zanzibar


Majenereta hayo yenye ambayo yamekwishatumika yenye thamani ya dola 250,000 yamekabidhiwa kwa Taasisi hiyo ili kusaidia jitihada za Chuo hicho katika kuhakikisha wanafunzi wanaendelea na masomo yao kipindi ambacho Umeme umekatika.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano mwishoni mwa juma mjini Unguja, Mkuu wa Kampuni ya Zantel, Zanzibar, Ndugu Mohamed Mussa Baucha alisema mchango huo una lengo la kuwasaidia wanafunzi wa chuo na masomo yao kama mbadala wa nishati hasa kipindi Umeme unapokua umekatika huku akitumai kwamba wanafunzi wa chuo hicho, watahimizwa kufanya vizuri kutokana na msaada huo.

"Ni jambo la furaha na faraja kwetu kutoa msaada wa majenereta kwa Taasisi hii, na tumaini letu kubwa ni kuwa yatakuwa msaada muhimu kwa wanafunzi katika masomo yao," alisema Baucha.

Aliongeza kuwa ZANTEL imekuwa msatari wa mbela katika kujitolea na itaendelea kuwekeza katika miradi mbalimbali endelevu na kuunga mkono mipango inayozingatia kuboresha elimu nchini.

Abdulhamid Idrissa Haji, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo alisema kuwa msaada huo umekuja kwa wakati muafaka kwa sababu chuo chake hakikuwa na vyanzo mbadala vya nishati, mara umeme unapokuwa umekatika, kitu ambacho kiliwasababishia wanafuzi wengi usumbufu.

"Ukosefu wa umeme vyuoni, hukatisha morali ya wanafunzi hasa hasa kwa masomo ya sayansi na uwezo wa kuyaelewa masomo hayo kwa usahihi."

Aliishukuru Zantel kwa msaada wao muhimu katika kuboresha ubora wa elimu nchini na kuhimiza makampuni mengine kufuata mfano huo.

“Msaada huu sio chachu tu katika ufaulu wetu kitaaluma bali pia utaongeza morali kwa wanafunzi,” alihitimisha Haji.

Mwanafunzi wa chuo hicho aliyefahamika kwa jina Abdulkadir Mkubwa Khamis ambaye anachukua masomo ya sayansi, alisema mchango wa Zantel utawawezesha kuboresha utendaji wao na pia kutatua baadhi ya changamoto ambazo zilikuwa zinawakabili hapo awali.

"Matatizo ya umeme huathiri sana masomo yetu, lakini kwa msaada huu, natumai matatizo hayo yatapungua," alihitimisha.

Mwaka jana, Kampuni ya Zantel ilitoa vitabu vyenye thamani ya 10M/- kwa Taasisi hiyo katika jitihada za kupunguza uhaba wa vifaa vya kufundisha na kujifunzia chuoni hapo.

Kwa maelezo zaidi, tutumie ujumbe

Angalia Kama Unapata Huduma

Tafuta duka la Zantel