Zantel Yakabidhi Kwa Mara ya Kwanza Zawadi Kuu ya Kampeni Yake ya ‘JERO YAKO TU’


Machi 5, 2018, Dar es Salaam. ZANTEL leo imekabidhi gari aina ya Toyota Suzuki Carry kwa mshindi wa kwanza wa zawadi kuu baada ya mshindi huyo kushiriki kikamilifu kwenye kampeni inayoendelea ya Kampuni hiyo ya 'Jero Yako Tu!'.

Hafla ya utoaji wa zawadi hiyo kubwa imefanyika katika ofisi za makao makuu ya Zantel jijini Dar es Salaam ambapo ilimshuhudia ndugu Mohammed Twaha (40) mfanyabiashara na mkazi wa Kinondoni akiondoka na zawadi ya kwanza ya kubwa katika kampeni hiyo. 

Pamoja na zawadi hiyo kuu kwa mshindi huyo, wengine  waliojinyakulia zawadi kabambe  ni pamoja na ndugu Masoud Juma Haji ambaye alishinda pikipiki, na Swalahu Ibrahim, Rashid Suleiman Rashid na Salum Hamadi Simai ambao waliojishindia zawadi ya baiskeli  katika kundi la zawadi za kila wiki. Wengine walikuwa Nyakungu Kinanda na Juzza Moiz ambao wote walishinda smartphone ya Moto C 4G.

Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa zawadi hizo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Sherif El Barbary alisema, "Tunafurahi kukabidhi zawadi yetu kubwa ya kwanza na tuna imani kwamba itawahamaisha wateja wengine wa Zantel kuendelea kushiriki katika promosheni hii inayoendelea ili waweze kuibuka na ushindi. Itakuwa ni fahari kubwa kuona sura mpya zaidi za watumiaji wa mtandao wa Zantel wakijishindia zawadi mbalimbali kama hawa wenzao. "

El-Barbary alibainisha kwamba Suzuki Carry hutumiwa zaidi kwa biashara hapa nchini Tanzania na kwamba utafiti mdogo ambao wameufanya umebaini kuwa wamiliki hupata pesa nzuri, na takwimu ya harakaraka inaonyesha wamiliki hao huingiza kati ya 25,000 / - 30,000 / - kwa siku na kupata karibu 900,000 / - kwa mwezi ambayo ni takriban 10.8m/ - kwa mwaka.

 Alisema Zantel pia itasaidia gharama za usajili, leseni ya barabara na bima ya mwaka mzima kwa washindi wake wote wa vyombo vya moto.

Kwa upande wake, Mtaalamu wa Idara ya Data na Vifaa Zantel, Bwana Hamza Zuheri alisema, tangu promosheni ilipoanza Januari 15, walikuwa wamepokea maombi ya washiriki wa promosheni hiyo takriban watu 250,000 huku takwimu ikionyesha idadi hiyo itaongezeka zaidi. Bw. Zuheri alisema kuwa kwa siku ya kawaida, takribani watu 5,000 hununua muda wa maoangezi kwa ajili ya kushiriki kwenye shindano hilo.

Kwa mujibu wa Zuheri, alisema lengo la promosheni ya 'JERO YAKO TU' inalenga kutoa zawadi na kuwashukuru wateja wa Zantel baada ya mafanikio ya marekebisho ya mtandao mpya wa kisasa na kuzindua mfumo wa 4G takribani katika mikoa 22 nchini Tanzania.

"Hatuoni njia yoyote nzuri ya kusherehekea mafanikio haya zaidi ya kufanya hivyo na watu ambao wametufikisha hapa, hususan wateja wetu waaminifu," alisema Zuheri.

Aliwakumbusha wateja wanaoshiriki katika promosheni hii kuwa ni rahisi sana, wanachopaswa kufanya ni kununua muda wa maongezi wa kiwango cha kuanzia Sh.500 na moja kwa moja wataingia kwenye droo. Hata hivyo, aliongeza kuwa, ili kujiwekea nafasi ya kushinda zawadi kubwa, mteja anatakiwa kushiriki mara nyingi zaidi.

Aliongeza kuwa zawadi za promosheni ni kuanzia simu za 4G na pesa taslimu 50,000 ambazo zinashindaniwa kila siku, pikipiki na baiskeli 4 ambazo zinashindaniwa kila wiki na  Toyota Suzuki Carry ambayo ni zawadi kuu inayoshindaniwa kila mwezi.

ZANTEL daima imedhamiria kuwaweka wateja wake mbele kwa kuwapa teknolojia za kisasa pamoja na ubora wa mtandao wa kuaminika na kuwa mtandao bora unaotoa huduma za data nchini.

 

Angalia Kama Unapata Huduma

Tafuta duka la Zantel