Zantel Wafanya Usafi wa Soko la Samaki Kunduchi


 

Hivi karibuni wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Zantel wameshiriki katika zoezi la usafi wa ufukwe wa bahari, ikiwa ni moja kati ya harakati za kampuni hiyo kuwajibika na kujitoa kwa jamii. Zoezi hilo lilifanyika katika soko la samaki la ufukwe wa Kunduchi mahala wananchi wanapofanya biashara zao za kuuza na kununua samaki.

 Kupitia zoezi hili Zantel ina lengo la kuhamasisha wananchi kuwa na utamaduni wa kusafisha fukwe za bahari, kuhifadhi mazingira pamoja na kuelimisha jamii kuhusu madhara ya uchafu na takataka kiujumla.

Mara kwa mara wananchi wamekua wakitegemea fukwe za bahari  kama sehemu za kupumzikia, kufurahia na pia kama chanzo cha chakula kama samaki lakini bado wamekua ni chanzo cha uchafuzi wa mazingira hayo wakiyafanya kama mahala pa kutupa takataka za aina mbali mbali.

Akiwakilisha kitengo cha raslimali watu , Bw. Frank Jackson mkuu wa kitengo hicho amesema “ Tunatumai kuelimisha jamii  kupitia mpango huu wa usafi na kufanya kila mmoja wetu kuwa na ufahamu nalo, ninaamini tunaweza kuleta mabadiliko ya ukweli, kuhamasisha kizazi kijacho kujali na kuzipenda fukwe za bahari na mazingira yote kiujumla kwaajili ya baadae”

Mpango huu unalenga kuleta mazingira safi na salama lakini zaidi ni kuleta manufaa kwa jamii ya Kitanzania kwa kuboresha biashara za ndani , utalii utakaopelekea kuongezeka  kwa  ajira, mazingira bora kwa wanyama na mimea, makazi mazuri kwa Wanyamapori na kiujumla kutengeneza jamii inayoweza kujivunia.

Kampuni ya mtandao ya Zantel inalenga kuunga mkono jamii zinazozunguka maeneo ya visiwani na bara katika jitihada za kuhamasisha umoja na utamaduni wa kujali watu wote. Mbali na jitihada za usafi kampuni ya mtandao wa Zantel inatarajia pia kufanya shughuli nyingine nyingi zaidi kwa jamii.

Kwa maelezo zaidi, tutumie ujumbe

Angalia Kama Unapata Huduma

Tafuta duka la Zantel