JARIBIO LA DHARURA LA AFYA NA USALAMA MAKAO MAKUU YA ZANTEL


 Ijumaa  saa nne asubuhi  kampuni ya ZANTEL PLC pamoja na timu ya Afya na Usalama ilibuni na kuandaa dharura inayosababishwa na tukio la moto lililotokea makao makuu ya Ofisi za ZANTEL. Moto ulianzishwa majira ya saa nne na dakika saba asubuhi kutoka kwenye takataka (matambara na matairi chakavu ya gari) ambavyo viliachwa  karibu na mfereji wa maji mbele ya ofisi za Stoo za Zantel. Moto uligunduliwa na mfanyakazi mmoja wa Zantel; Khamis Bakar Khamis ambaye ni Meneja wa Mipangilio ya Data ambaye alikuwa akielekea kwenye stoo

Baada ya kubaini moto, Khamis kwa haraka alikwenda kwenye kengele ya miito ya dharura na kubonyeza kengele hiyo kuashiria hali ya hatari. Baada ya milio ya kengele kusikika wafanyakazi wote waliondolewa kwa haraka haraka kutoka maofisini na kuelekezwa kwenye uwanja wa dharura wa kukusanyikia pamoja kwa tahadhari pindi inapotokea dharura yeyote. Wakati huo huo mkufunzi wa moto, kutoka kitengo cha Mauzo na Usambazaji; ndugu Hamid Mohamed Bakar ambaye alikuwa akizunguka eneo hilo kutoka kwenye chumba cha chini cha ofisi za Zantel, pamoja na Amiri Damas (msimamizi wa moto wa Zantel) aliweza kuuzima moto huo kwa wakati kwa kutumia kifaa maalum cha kuzimia moto.

Lengo la zoezi hili lilikuwa ni Kupima ufahamu wa wafanyakazi kuhusu taratibu za uokoaji wakati wa dharura. Pili ni kupima ufanisi wa moto na vituo vya dharura / mifumo iliyowekwa katika ofisi ya ZANTEL na kupima majibu ya mamlaka ya dharura na uokoaji kama vile Vikosi vya zima moto, Magari ya dharura kwa wagonjwa nk. Kama sehemu ya maandalizi ya dharura hii ni kuwakumbusha wafanyakazi wote uzingatiaji na utekelezaji wa taratibu za dharura ili kuepuka athari katika kesi ya tukio lolote au lile linaloweza kutokea katika maeneo yetu ya kazi na pia  kuamsha Mamlaka  za zima moto na Magari ya dharura ya Hospitali katika kutekeleza wajibu wa majukumu yao katika kuitikia miito pindi dharura inapotokea.

Kwa maelezo zaidi, tutumie ujumbe

Angalia Kama Unapata Huduma

Tafuta duka la Zantel