Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel leo imetanga viwango vipya vya bei vya kupiga simu kwa wateja wake wa
malipo ya kabla. Viwango hivyo ni Tsh 1 kwa sekunde Zantel kwenda Zantel masaa 24 popote Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari Afisa Mkuu wa Biashara Bw. Faisal Khan amesema dhumuni la kuzindua
viwango hivy ni kuwawezesha wateja wake kupata huduma za mawasiliano nafuu na hivyo kutimiza ahadi ya kampuni
yake ya kuwawezesha Watanzania kuongea zaidi.
“Zantel inajulikana kuwa ni mtandao unaowapa wateja thamani kwa fedha zao na ukiwa ni mtandao ulionea
zaidi hapa nchini, viwango hivi vipya vitaimarisha msimamo wetu wa kuwa mkobozi wa wateja katika sekta ya
mawasiliano hapa Tanzania”, alisema Bw. Khan.
‘Ukiwa ni mtandao ulioenea zaidi nchini kwa sasa, viwango vya bei tunavyozindua leo hakika vitawawezesha wateja wetu
kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki wakiwa popote Tanzania kwa gharama nafuu kabisa’ ameongezea Bw. Khan.
Kuweza kujiunga na viwango hivi vipya mteja wa Zantel anatakiwa kujisajili bure kwa kupiga *145#
Zantel is inajivunia kuwa na mtandao ulionea zaidi hapa nchini pamoja na kwamba ni mtandao wa mwisho kuingia kwenye
soko la Tanzania. Mtandao wa Zantel umeenea sana katika mikoa, miji na vitongoji vingi zaidi hapa nchi.
Vile vile mtandao wa Zantel unapatika katika bara bara zote kuu hapa nchini kuhakisha kuwa hata kwa wale wanousafiri
wanafaidika na huduma zao wakiwa popote nchini.
Dhumuni kubwa la Zantel ni kuhakikisha kwamba Watanzania wote wanafaidika na kufikiwa na huduma za
mawasiliano zenye gharama nafuu.